BWANA YESU AMETUAGIZA MAOMBI

BWANA YESU ASIFIWE....
Maombi yana nguvu ya kubadili mazingira magumu yakawa marahisi.Tukiwa ndani ya maombi Bwana Yesu ametuamuru tuombe wakati.
Bwana Yesu alisema tukeshe katika kuomba maana saa atakaporudi yeye hatujui.
35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jimbi, au asubuhi
36 asije akawasili ghafula akawakuta mmelala.
Marko 13 :36
37 Na hilo niwaambialo ninyi, nawaambia wote, Kesheni.
Marko 13 :37
2.Ombeni msije mkaixxx ngia majaribuni.
Hili ni agizo la Bwana Yesu kwa waliofanyiwa wanafunzi wake. 41 Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni; roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.
Mathayo 26 :41
3.Omba kwa ajili ya watenda kazi.
Kati ya maagizo tuliyopewa na Bwana Yesu ni kumwomba Bwana wa mavuno kuleta watenda kazi... Mavuno ni mengi watendakazi wachache. 2 Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake.
Luka 10 :2
3 Enendeni, angalieni, nawatuma kama wana kondoo kati ya mbwa-mwitu.
Luka 10 :3
4.Omba kwa ajili ya wenye mamlaka.
Wenye mamlaka wanatakiwa kuombewa sana,tusipowaombea shetani atawavuruga wakatuumiza.
1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
1 Timotheo 2 :1
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
1 Timotheo 2 :2
3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;
1 Timotheo 2 :3
4 ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.
1 Timotheo 2 :4
5.Kuwaombea ombea maadui.
Mara nyingi wenye maombi hatupendi kuwaweka wale waotutuudhi. Lakini Yesu Kristo ametuagiza kupendana na kuwaombea wanaotuudhi.
28 wabarikieni wale ambao wawalaani ninyi, waombeeni wale ambao wawaonea ninyi.
Luka 6 :28
6.Kuwasamehe waliotukosea.
Bwana Yesu alisema tuwasamehe kila yanapoanza24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Marko 11 :24
25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Marko 11 :25
26 Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
Marko 11 :26
maombi. 24 Kwa sababu hiyo nawaambia, Yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.
Marko 11 :24
25 Nanyi, kila msimamapo na kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu.
Marko 11 :25
26 Lakini kama ninyi hamsamehe, wala Baba yenu aliye mbinguni hatawasamehe ninyi makosa yenu.]
Marko 11 :26
Maoni
Chapisha Maoni