NENO LA BWANA KINYWANI MWANGU
Bwana Yesu asifiwe....
Neno la Mungu ni wazo la Mungu ambalo huwekwa katika mawazo ya Binadamu na kutamkwa kwa watu ili kuwasaidia na kuwatoa katika maangamizo yao. Neno la Mungu lililoandikwa limetamkwa na Mungu kwa njia ya watumishi wake na kuandikwa katika Kitabu kiitwacho BIBLIA. Hata sasa Mungu anazungumza na watu wake kwa njia mbalimbali ili kuwasaidia. Neno hilo humjia MTU kwa njia ya Ufunuo kwa kuwekwa wazikwake kwa nguvu na ushawishi Mkubwa. Neno la Mungu ni Tofauti na maneno ya wanadamu kwani Neno la Bwana ni Roho tena ni kweli huwatoa watu katika maangamizi yao.
NENO LA MUNGU KINYWANI MWAKO.
Mungu Baba huweka Neno kinywani mwetu ili kutusaidia na kututoa katika maangamizi yote.(“Mwanamke akamwambia Eliya, Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la Bwana kinywani mwako ni kweli”)
1 Wafalme 17:24 Mama mjane wa Serepta katika Mji wa Sidoni alikubali kuwa Neno la Bwana kinywani mwa Eliya ni kweli na Imetimizwa maishani. Hivyo kila anayetumika awe amejazwa Bwana Neno lake, maana Hakuna Nabii, Mwalimu, Mtume, mwunjilisti, mchungaji wa kweli aliyenena Neno lake mwenyewe Bali Neno la Mungu katika maisha ya watu ili watu wapone.

Isaya 6
⁷ akanigusa kinywa changu kwa kaa hilo, akaniambia, Tazama, hili limekugusa midomo yako, na uovu wako umeondolewa, na dhambi yako imefunikwa.
⁸ Kisha nikaisikia sauti ya Bwana, akisema, Nimtume nani, naye ni nani atakayekwenda kwa ajili yetu? Ndipo niliposema, Mimi hapa, nitume mimi.

Yeremia 1
⁷ Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru.
⁹ Ndipo Bwana akaunyosha mkono wake, akanigusa kinywa changu; Bwana akaniambia, Tazama, nimetia maneno yangu kinywani mwako;
¹⁰ angalia, nimekuweka leo juu ya mataifa na juu ya falme, ili kung'oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza; ili kujenga na kupanda.
Kutoka katika mifano hii miwili tunajifunza Mungu aliwatengeneza watumishi na kuweka Neno kinywani mwao. Hakika kila Nabii wa Agano la kale na mitume wa Agano Jipya hawakujihubiri wenywe Bali Neno lake Bwana vinywani mwao. Leo kuna watu wanabeba maneno tofauti na Neno la Bwana.
NENO LA MUNGU NI UPANGA.
Kama upanga Mkali mkononi mwa shujaa ndivyo livyo Neno la Mungu kinywani mwa mtumishi wake. Neno litakata kila aina ya uwongo wa shetani ulio maishani mwa mtu anayeokolewa. NENO La Mungu ni upanga mkali sana katika kukata na kugawanya kila neno la Mwanadamu.
“Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Waebrania 4:12
Waebrania 4:12
NENO LA MUNGU NI MOTO NA NYUNDO
“Je! Neno langu si kama moto? Asema Bwana; na kama nyundo ivunjayo mawe vipande vipande?” Yeremia 23:29
Neno la Mungu ni moto na nyundo kuchoma na kuvunja vitu ambavyo havitokani na Mungu wa mbinguni. Katika mambo yote ambayo unaweza kukutana kama umejaa Neno na ahadi za Mungu ni sawa na aliyebeba moto na nyundo kuvunja manabii wa uwongo na mafundisho ya mashetani. Na kupanda Mafundisho ya Yesu kristo.

NENO LA MUNGU NI UZIMA.
Neno la Mungu ndani limebeba uzima wa roho, mwili,nafsi na kuchumi. Neno la Bwana lina uzima katika maisha ya Binadamu na viumbe vingine kwa sababu vyote vyote viliumbwa kwa Neno la Bwana.
“Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.''Yohana 6:63
Mtumishi aliyebeba Neno Mungu anapotamka Neno la Mungu uzima unatokea haraka sana. Eliya alimfufua mtoto wa mama wa Serepta baada ya kufa, Elia alitamka Neno la Mungu ili roho imrudie na Ikiwa hivyo. Pengine unaposoma kitabu hiki kuna kitu kinataka kufa au kimechoka sana. Inua macho yako kwa kuamini Neno la Mungu aliyehai nawe utapona magonjwa yako.

1 Wafalme 17 ¹⁹ Akamwambia, Nipe mwanao. Akamtoa katika kifua chake, akamchukua juu chumbani mle alimokaa mwenyewe, akamlaza kitandani pake.²² Bwana akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka²⁴ Mwanamke akamwambia Eliya, Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la Bwana kinywani mwako ni kweli.
Maoni
Chapisha Maoni